Friday, August 24, 2012

DORTMUND WAANZA VIZURI KUTETEA UBINGWA WAO WA BUNDESLIGA





Picha ikionyesha shamrashamra zilivyotawala mjini Dortmund wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya mpira wa miguu Ujerumani (Bundesliga), ambaopo  mabingwa watetezi Borussia Dortmund waliwapa kichapo maridadi Werder Bremen cha Magoli mawili kwa moja.

Thursday, August 23, 2012

KITALE NI NOMAAA!!!!!! HILI DUDE NOMA LINACHEZWA MTONI MPAKA KIGOMA

BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO KITAKATIFU "ZOLA D" ATOA SABABU LUKUKI




Sijui ni mila, utamaduni, desturi, kawaida au mazoe kwa wanamichezo wa Tanzania wanaposhindwa huwa hawakubali kama wameshindwa kihalali na badala yake kutoa vijisababu vya ajabu ajabu, hayo yalikuwa maneno yaliyotolewa na mmoja kati ya mashabiki waliohudhuria mpambano wa masumbwi kati ya Zola D ambaye pia ni mwanamuziki wa bongo fleva na Mchumia Tumbo.

Shabiki huyo alifyatuka maneno hayo baada ya kusikia maneno ya Zola akijitetea eti kuwa ulingo ulikuwa umelowa maji na ndio sababu ya yeye kuanguka wakati alipojaribu kumshambulia mpinzani wake. "Inamaana kama ulingo ulikuwa na maji, huyo mchumia tumbo alipigana na mtumbwi au boti?" aliendelea kuropoka shabiki huyo. Huku sauti kutoka kwa shabiki mwingine ikisikika akisema " basi na yeye Zola angepewa ngalawa" kisha wote wakacheka na kukata simu.

Hapo ndipo ukawa mwisho wa mahojiano yangu na wadau hao, kama una maoni unaweza kuyasogeza kupitia:  djmaxentertainments@yahoo.de


AFYA YA BI KIDUDE SI NZURI KWA SASA, AUGUZWA NA MJUKUU WAKE NYUMBANI KWAKE ZAZNZIBAR




Mwanamuzi mkongwe duniani bi kidude, amabae ni mzaliwa wa Zanzibar Tanzania kwa sasa yuko kitandani amabapo bado haijajulikana rasmi anasumbuliwa na maradhi gani (daktari hajathibitisha). Tangu alipoanza kutojisikia vizuri kwa zaidi ya wiki sasa yupo tu nyumbani kwake akiuguzwa na mjukuu wake.

Utafiti wa kitaalam wala msada wa kitaalam hajapatiwa pia hakuna mdau yoyote wa muziki kutoka nchini Tanzania wala bara la Afrika aliyefika kumjulia hali mpaka sasa, hayo aliyasema mjukuu wake wakati alipokuwa akitoa malalamiko yake kupitia sauti ya Tanzania Zanzibar.

Kwa niaba ya "The Dj Max Entertainments" tunamuomba Mungu amuondolee maradhi na amrudishie afya yake apate kuwa mzima na kuendeleza gurudumu la muziki kama kawaida. Mwenyezimungu atampa bibi yetu afueni "AMEEN"

MAY D APIGWA CHINI P SQUARE RECORDS




Tetesi zimezagaa kuwa kuna kutokuelewana kati ya uongozi wa P square records na msanii May D ambae pia ni kutoka Nigeria kitendo ambacho kimesababisha msanii huyo kuenguliwa kwenye lebo hiyo. Mwenyewe May D anasema hana taarifa hizo rasmi kutoka kwa uongozi wakati wadaku wa karibu wanasema msanii huyo hajawahi kufanya makubaliano ya kimaandishi na lebo hiyo, yalikuwa ni makubaliano ya kiushkaji tu kwa njia ya mdomo.

May D ni msanii kutoka Nigeria ambaye alimeremeta vizuri sana kwenye "vesi" ya pili ya wimbo wa "Chop my money remix" na kuonyesha uwezo wa hali ya juu aliposhirikishwa na mabosi zake hao wa P square

Tuesday, August 21, 2012

PROMOTA WA MAJUU NA PROMOTA WA BONGO USO KWA USO




Muandaa matamasha maarufu barani Ulaya mtanzania anaeishi Norway Hassan Nganzo ambaye pia anafahamika kwa jina la kaka mkubwa, ikiwa ni heshima anayopewa na wadau wa muziki na burudani barani Ulaya (mwenye shati jeupe wa kwanza kushoto) Juzi kati mnamo wiki ya mwisho ya mfungo alipata wakati wa kupiga story na Saidi Fella (mwenye fulana ya blue, wakwanza kulia) katika hafla ya futuru iliyoandaliwa na kundi la Tiptop connection la Manzese Dar.

Baada ya kalamu hiyo ambayo pia iliwakutanisha Abdul bonge na Babu Talle (mwenye fulana nyekundu) wadau hao wa muziki wa kizazi kipya walipata muda wa kujadiliana mawili matatu juu ya changamoto zinazowakabili waandaji wa matamasha Afrika na Ulaya ikiwa sasa kuna vuguvugu la baadhi ya wasanii kujihusisha na vitendo vya kitapeli, hasa wasanii wa bongo fleva.

Hassan Nganzo (kaka mkubwa) yupo Tanzania sasa kwa ziara ya kikazi na mapumziko mafupi, tunamtakia kila la heri na pia atuwakilishe vyema wadau wa muziki wa kizazi kipya barani Ulaya

SHETTA AJITOA DARSTAMINA, KUANZISHA KUNDI LAKE




Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania sheta ameamua kujitoa na katika kundi la Darstamina, hatimae amaemua kuanzisha kundi lake litakalokwenda kwa jina la shettateam. Sheta aliweka wazi dhamira yake hiyo kinaga ubaga alipokuwa akipiga stori na Dj Fetty pia amesisitiza kuwa ataweka wazi sababu za kujitoa kundi la Darstamina hivi karibuni.

Wednesday, August 15, 2012

TUNDA MANA ARUDIA "SHOOTING" YA WIMBO WA DEMU SIO BAADA YA VIDEO YA KWANZA KUONEKANA KUWA HAINA VIWANGO




Tunda Man akiwa katika harakati za kufanya video hiyo kwa mara ya pili baada ya mashabiki kudai kuwa ile ya kwanza haina viwango pamoja kuwa aliifanya kwa director machachari bongo Adam Juma

UP COMING STAR "BOBBY ST" LIVE in MUNICH on 1st SEPTEMBER 2012





Msanii anaekuja juu kwa kasi mwenye asili ya Kenya ambae anaishi ujerumani, anatarajiwa kutoa burudani ya  aina yake kwenye tamasha kubwa la kihistoria (EAST vs WEST AFRICAN PARTY vol 2). Ambalo limeandaliwa na the Dj Max Entertainments kwa kushirikiana na Shounkemp Int. Studio Jay Musik.

Pia kutakuwa na burudani mbalimbali za muziki siku hiyo ambapo ma Dj wakali kutoka East an West Africa watakuwa wakionyesha uwezo wa kuchezea mashine.

Kutoka East safu ya muziki itaongozwa na Dj Rama, Dj Dully boy na mwanadada machachari Dj Lady Kiarie. Vilevile kama afya ya mkono itaendelea vizuri Dj Max nae atarejea ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa mkono kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Wakati upande wa West burudani itatolewa na Dj Korea, Dj Timberland bila kumsahau Dj Jay, kila mtu anakaribishwa kula bata



Sunday, August 12, 2012

FC BAYERN KUFUTA UTEJA KWA DORTMUND LEO?????




Ikiwa ni misimu miwili mfululizo na kwa zaidi ya mechi tano, Fc Bayern watoto wa kibavaria wameshindwa kabisa kuonyesha makali yao dhidi ya nyuki wa Dortmund pamoja na kuwa na kikosi kinachoogopewa zaidi nchini ujerumani huku wakiwa wamekusanya zaidi ya nusu ya mastaa wa timu ya taifa ya ujerumani.

Leo saa mbili usiku kwa saa za ujerumani na saa tatu kwa saa za Afrika mashariki vigogo hao wataingia uwanjani katika fainali ya kombe la "Super cup" ambayo itapigwa ndani ya Alllianze Arena, uwanja wa nyumbani wa Fc Bayern. Swali la msingi je Bayern bado wataendelea kuwa vibonde????

Thursday, August 9, 2012

Wednesday, August 8, 2012

EVENT OF THE YEAR SEPTEMBER 1st 2012 in MUNICH





Its a big time when Brothers and sisters from all over Africa coming together and Enjoying the Music together from Best DJs in Germany. Drinking and having Fun together with our German friends and some other friends from all over the world

EAST vs WEST AFRICAN PARTY

WELCOME ALL!!!!!

Sunday, August 5, 2012

WERDER BREMEN MABINGWA WA LIGA TOTAL UJERUMANI





Wachezaji wa Bremen wakifurahia ushindi baada ya kuwakunyuga mabingwa wa ligi ya ujerumani "Bundes Liga" Borussia Dortmund kwa mikwaju ya penat katika mchezo wa fainali uliofanyika jioni ya leo.

Pia kulikuwa na mchezo mwingine wa kutafuta mshindi watatu ambapo Fc Bayern München (champions of the heart) waliwaadhibu mabaharia wa Hamburg kwa kuwachapa kidude

KENYAN PROUD: EZEKIEL KIMBOI WON GOLD MEDAL




Bwana Kimboi akifurahia ushindi kwa kucheza "style" ya kuzungusha.
zungusha!!!!   zungusha!!!!! zungusha ndugu!!!!!

PROFESSOR JAY AWAKANYA WANAOMZUSHIA KIFO DIAMOND PLATNUMZ "MNYAMA"





(Diamond alipokuwa Hospital akifanyiwa check up)

Msanii mkonngwe "Big daddy" Josseph Haule almaarufu kama Profesa Jay, jana aliandika kwenye face book wall yake kuwakemea wanaomzushia kifo msanii machachari Diamond Platnumz ukipenda unaweza kumwita Mnyama au raisi wa wasafi.

Diamond ni mzima wa afya na bado yuko ngangari anadunda mtaani hayo ni baadhi maneno yaliyoandikwa na mkongwe Jay katika ukuta wake wa uso kitabu jana.Pia aliwakemea watu waache tabia ya uzushi na udaku. Diamond hajafa ila alikuwa anaumwa tu kama binadamu mwingine yoyote anavyoweza kupatwa na maradhi.

Kwa niaba ya Dj Max Entertainments na wana Afrika mashariki wote wa hapa ujerumani tunamuombea afya njema mnyama Diamond na apone haraka

Friday, August 3, 2012

BOBBY ST: MKENYA ANAEISHI UJERUMANI AACHINGA VIDEO YA NGOMA YAKE MPYA "MAMACITA"

JAGUAR: NAMSAPORT PREZZO KWENYE BIG BROTHER KWA KUWA NI MKENYA MWENZANGU




Msanii maarufu Afrika mashariki kutoka nchini kenya JaguarKenya "Mzee wa kigeugeu" amefunguka na kusema kwa sasa anampa suport mshiriki kutoka kenya kwenye jumba la Big Brother Africa ambaye pia ni msanii kutoka Kenya "PREZZO"

Pia amekanusha kuwa amekuwa akitumia account yake ya "Tweetwer" kuwahamasisha funs wake wasimpigie kura Prezzo na kama star huyo atashinda basi yeye Jaguar atahamia nchini Uganda for good. "Mimi sina account ya tweeter na wala sio mimi niliandika message hizo, mtandao pekee ninaotumia ni face book. I suport Prezzo just because he is Kenyan like me" alisema Jaguar

Wednesday, August 1, 2012

PREZZO KUIBUKA MSHINDI BIG BROTHER AFRICA??? APEWA "SUPORT" NA WAZIRI MKUU WA KENYA BW. RAILA ODINGA




Mwakilishi wa Kenya ndani ya jumba la "Big Brother"ambaye kwa sasa anasimama kama mwakilishi wa Afrika Mashariki Prezzo anayepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi na mashabiki wengi, pia anapigwa tafu la nguvu na waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga ambaye amekuwa akiwahamasisha watu wampigie kura.