Friday, November 30, 2012

KITALE AWALAANI WALIOMFANYIA UBAYA SHARO MILIONEA



Swahiba wa karibu wa marehemu "Sharo" na pia ni mshirika wake mkubwa kwenye kazi za muziki na sanaa ya uchekeshaji "Kitale" Juzi alilaani vikali na kuwalaani waliomfanyia vitendo visivyo vya kibinaadam Sharo baada ya kupata ajali. Kitale aliongea kwa masikitiko na uchungu mkubwa alipokuwa akihojiwa na Millard Ayo wa Clouds Fm, "Watanzania hawana huruma, wamemvua marehemu mpaka viatu yani wamemuacha na nguo ya ndani tu" hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema Kitale.

Kiukweli kabisa kitendo hicho hakina hata chembe ya uungwana hasa ukizingatia ajali mbaya kama hiyo aliyoipata Sharo, watu badala ya kufika eneo la tukio nakutoa msaada badala yake wanaenda kufanya vitendo vya wizi na uhalifu. Pia kitale alisema kuwa marehemu wakati anaondoka alikuwa na jumla ya shilingi za kitanzania milioni 6 ambazo pia hazikupatikana. Huku akiwa na sura iliyojaa machungu kitale aliongea maneno hayo kwa huzuni alihani kana kwamba haamini kama ni kweli kampoteza swahiba wake.

Kwa niaba ya " THE DJ MAX ENTERTAINMENTS" tunaungana na kitale na waungwana wengine wote kulaani kitendo kisicho cha kibinadamu alichofanyiwa marehemu "Sharo".Pia tunalaani matendo kama hayo katika ajali nyinginezo. Vilevile tunatoa pole kwa Familia ya wafiwa, ndugu jamaa na Marafiki. Mungu ailaze pema roho ya Marehemu. Ameen!

Saturday, November 10, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH!!! AND THE WINNER IS WALTER CHILAMBO



Ni mzaliwa wa Mbeya na aliyekulia na kusomea mkoni humo, lakini alikuwa akiwakilisha mkoa wa Dar es Salaam katika shindano la kuimba la "Bongo Star Search" ambalo limefikia kilele masaa machache yaliyopita. Hakuna ubishi wala utata kuwa huyu ndiye mshindi na amejinyakulia kitita cha shilingi za kitanzania milioni 50  ikiwa inakaribia sawa na dola za kimarekani 50,000/=

HONGERA SANA WALTER 



Monday, November 5, 2012

MATONYA'S NEW VIDEO "ZILIPENDWA"

TUHUMA ZA DIAMOND PLATNUMZ KUIBA WIMBO WA H-BABA. Q CHIEF AFUNGUKA KUTOA USHUHUDA




Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, raia wa Tanzania al maarufu kama mzee wa kubembeleza Q chillah. Aliyetajwa kama shahidi katika malalamiko ya H-baba kuibiwa songi lake la "Nataka kulewa" na msanii Nassib Abdul (DIAMOND). Juzi kati mtu mzima Chillah alivunja ukimya alipokuwa akihojiwa na Radio ya watu Clouds fm na kutiririka. "Ni kweli tulikuwa katika maandalizi ya kurekodi wimbo huo na H-baba na mimi ndiye niliyeimba kiitikio na hata Diamond na Sheta walipokuja wakakuta tunaimba na kuupenda wimbo, lakini kwanini tugombane au kuanzisha mzozo kwa sababu ya wimbo? labda mawazo yaligongana tu. H-baba ni msanii mkubwa naamini ana uwezo wa kufanya ngoma nyingine." Alisema Q Chief.

kama umeusikia wimbo nataka kulewa wa Diamond ambao umezua utata basi ni nafasi yako kuusikia na wa H-baba ambaye analalamika kuibiwa wimbo huo ambao bado haujakamilika, kisha utapima mwenyewe.

 Banyoza HAPA kusikiliza


Saturday, November 3, 2012

"NATAKA KULEWA" NI WIMBO WANGU NA HATA DIAMOND ANAJUA. LAKINI AMEAMUA KUNIIBIA



(H- baba akiwa ameshika cd ya demo yenye wimbo huo kama ushahidi)

Namshangaa sana huyu bwana mdogo, alikuja studio kwa Maneke akiwa na Sheta wakati wanafanya ngoma yao ya nidanganye, wakanikuta mimi na Q chillah tunafanya wimbo wangu mpya (nataka kulewa) ambao nimemshirikisha Q chillah kwenye kiitikio. Diamond akasema ameupenda huo wimbo na akawa ananiambia nimuimbie kwani unamfurahisha nami nikawa namuimbia. Leo nasikia kautoa redioni wakati mimi sijamaliza kuuredi. Kama mnabisha muulizeni Q chillah au maneke. "hayo ndiyo malalamiko ya msanii Hamisi baba ambaye ni mkongwe kwenye fani ya muziki wa kizazi kipya. Pia aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha Diamond kuiba baadhi ya maneno katika kiitikio na jina la wimbo huo kimemsikitisha sana



Thursday, November 1, 2012

ALICHOKIONGEA BOB JUNIOR KUHUSU NGOMA MPYA YA DIAMOND "NATAKA KULEWA"




"Ni wimbo wa kawaida sana wala sijaona mabadiliko wala ubunifu, bila kuambiwa hata wewe utajua tu kuwa ni nani anaeimba". Maneno hayo aliongea rais wa Masharobalo na Bosi wa Sharobalo records bwana Bob Junior, alipokuwa akifanya mahojiano na Soud brown wa Clouds Fm. kwenye kipindi cha xxxL. Pia aliongeza kwa kusema kwa sasa nipo tayari kupimana nae nae uwezo kwani watu sio wajinga waangalia kipaji na sio majigambo

DAVID ALABA KUFUNGUA KESI DHIDI YA KITUO CHA T.V CHA "ORF" KWA KUMDHALILISHA



Mchezaji kinda ndani ya nyota nyekundu ya kusini "FC BAYERN" raia wa Austria mwenye asili ya mchangiko wa kiafrika na Asia (baba kutoka Nigeria na mama kutoka Ufilipino). David Alaba amepeleka malalamiko kwa mwanasheria wake na kutaka kufungua kesi dhidi ya kituo hicho cha nchini Austria kwa kitendo ambacho alikiona ni cha kudhalilisha na kumbagua. Kupitia kipindi chake cha Commedy, walimuonyesha mtu mweusi mwenye jezi ya Bayern akiwa na tajiri wa kizungu kutoka Canada.

Matukio yaliyomkera Alaba ni pamoja la tajiri huyo kumuonyesha ndizi (chakula cha nyani) Alaba, pia kumuuliza kama anaishi kwenye nyumba za ukimbizi au nyumba za mabati zilizoezekwa na nyasi. Pia mtu huyo alimuuliza Alaba kama ana elimu au amewahi kwenda shule kwa kuwa "Black man" anawaza hela tu. Hata hivyo kituo hicho cha TV kiliomba radhi kwa mchezaji huyo na kuweka wazi kuwa hawakuwa na lengo la kumdhalilisha. Mpaka sasa Alaba hajaonyesha bado dhamira yoyote ya kubadili msimamo wake juu wa kufungua kesi dhidi ya televisheni hiyo