Monday, July 30, 2012

Sunday, July 29, 2012

JOSE CHAMELEONE AINGIA CHOO CHA KIKE





Huu ni msemo wa watoto wa mjini ikimaanisha kwamba mtu amejiingiza mtegoni au amejikuta yupo mahala asipotaka kuwa kwa wakati ule. Hapa tunafananisha kitendo cha msanii Jose Chameleone kutoka Uganda kuingia kwenye bifu na bwana Eric Shigongo, ni sawa na kuingia choo cha kike.

Eric James shigongo ni mwandishi maarufu wa vitabu Afrika Mashariki pia ni mmiliki wa kampuni ya Global Publishers ambayo inachapisha magazeti, ya Ijumaa, Amani, Uwazi, Champion pamoja na mengineyo nisiyoyajua mimi. Wachambuzi wa  mambo wanaweka swali bayana je magazeti ya Shigongo yatakuwa yakiandika nini kuhusu msanii Chameleone??? na sote tunatambua nguvu ya vyombo vya habari.

kwa niaba ya The Dj Max Entertainments tunakilani kwa nguvu zote kitendo cha utapeli kilichofanywa na msanii Jose Chameleone na wngineo wenye tabia kama yake tunawalaani pia. Kwani wasanii wa Afrika Mashariki wengi wamekuwa wakijiingiza katika utapeli wa namna hii na tutawafichua mmoja baada ya mwingine.

Saturday, July 28, 2012

JOSE CHAMELEONE NI TAPELI??? YASEMEKANA KUWA ANAFANYA KAZI ZAKE KWA UBABAISHAJI SANA!!!




AMEWAHI KUMPIGA CHANGA LA MACHO DJ JAY DEE

Dj Jaydee (Johhn Dillinga Matjor) muandaaji wa matamasha nchini Tanzania ambae pia aliwahi kufanyiwa utapeli na msanii Jose Chameleone mwaka 2005.

Sakata la msanii Jose Chameleone kutoka Uganda kuchuliwa hati yake ya kusafiria "Passport" na muandaaji wa matamasha ambae pia ni mmiliki wa kampuni ya Global Publisher, "the big name" Eric James shigongo lachukua taswira mpya. Ni baada ya mashuhuda lukuki kujitokeza na kutoa ushuhuda wao juu ya vitendo vya kihuni walivyofanyiwa na msanii huyo. 

Moja wa mashuhuda hao ni mtabgazaji wa radio na Dj maarufu nchini Tanzania mwenye asili ya South Africa Dj Jaydee, ambaye pia ni muandaaji wa matamasha.Dj Jaydee alitoa ushuhuda wake mbele ya waandishi wa habari hapo jana jijini Dar es Salaam.

ERIC SHIGONGO NAE AFUNGUKA KUHUSU "SKENDO" YAKE NA MSANII JOSE CHAMELEONE

Friday, July 27, 2012

HIVI NDIVYO CHAMELEONE ALIVYOOMBA MSADA WA KUPEWA PASSPORT YAKE NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA




Kitendo cha msanii Jose Chameleone wa Uganda kuchukuliwa Passport wake na muandaaji maarufu wa matamasha nchini Tnzania bwana Eric Shigongo chazua maswali mengi na mijadala. Je? wasanii wetu wa Afrika Mashariki wamekuwa matapeli? hawaridhiki na kipato chao? ni roho mbaya tamaa au wivu?

Inasemekana Chameleone kashawahi kufanya mambo kama hayo nchini Holland mpaka akashikiwa bunduki na muandaaji wa tamasha ndipo akapanda jukwaani. Pia aliwahi kufanya hivyo Belgium mwaka 2007, alipochukuwa hela za show na kuingia mitini. Na hivi sasa tayari kashachukua "advance" ya show kibao za majuu ambapo mojawapo inatarajiwa kufanyika Belgium jumamosi ijayo. Je atakuja????

MSANII JOSE CHAMELEONE ATOA UFAFANUZI KUHUSU SAKATA LAKE LA KUCHUKULIWA PASSPORT YAKE NA ERIC SHIGONGO

Thursday, July 26, 2012

ARBA WA KUKAYE MOTO BAND KUWASHA MOTO NDANI YA TUPO PAMOJA FESTIVAL IN NÜRNBERG JUMAPILI HII





Kazi ya ubunifu ikionyesha jinsi ratiba ya shughuli nzima itakavyokuwa, ambapo mwanamuzi maarafu wa kitanzania anaeishi Ujerumani kutoka kwenye kundi la Kukaye Moto pia ataonyesha manjonjo yake.

 Ikumbukwe kuwa tamasha hili ni kwa ajili ya kukusanya vifaa vya michezo na muziki kwa ajili ya watoto waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu. Lengo ni kuendeleza vipaji vyao ili waweze kujitegemea baadae. Vilevile kukusanya michango kwa ajili ya walimu na walezi kuweza kujikimu kimaisha.




Muandaaji wa shughuli hiyo na pia mlezi wa watoto Bwana Eric Moro akiwa na wageni waliomtembelea katika banda lake kwenye maonyesho ya Tamasha la kiafrika (Afrcan Festival) Nürnberg mwezi "June" Mwaka huu.

Tamasha la kujitolea Nürnberg linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii 29-July-2012 siku ya jumapili kuanzia saa saba za mchana katika mji wa Nürberg nchini Ujerumani.

Nyote mnakaribishwa kwa kiingilio cha bure

Wednesday, July 25, 2012

WACHINA KWELI NOMA!!! WAWAVALISHA FC BAYERN JEZI ZA KICHINA KWENYE ZIARA YAO NCHINI HUMO


Baadhi ya wachezaji wa FC Bayern wakiwa kwenye benchi la ufundi na jezi zao zenye majina ya kichina, kutoka kushoto ni Mario Gomez, Thomas Müller na Holger badstuber.

Jionee mwenyewe jinsi maina yao yalivyoandikwa kichina, Bayern walicheza jana mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao wa Beijing na kuwakandamiza magoli 6 kwa sifuri bila huruma.

Monday, July 23, 2012

FC BAYERN CAMPING IN BEIJING CHINA WITHOUT CAPTAIN LAHM AND SCHWEINSTEIGER


Kikosi kamili cha timu ya Bayern Munich kilipowasili mjini Beijing China bila ya Manahodha wake Philipp Lahm na Bastian Schweisteiger.

 Sababu za kuwaacha mastaa hao ni kuwapa mapumziko kwa kuwa Lahm amecheza mechi nyingi sana mfululizo kwa zaidi ya miaka miwili. Pia Bastian anapumzishwa kutokana na kuumia mara kwa mara, ingawa wawili hao wameanza mazoezi ya peke yao katika uwanja wao wa nyumbani wa mazoezi uliopo maeneo ya "Säbener Str." jijini Munich, wakiwa chini ya waalim maalum wakipewa mazoezi maalum.



Kocha wa Fc Bayern Jupp Heynckes (mwenye jezi nyeusi) akiwa na wachezaji wapya aliowaongeza kwenye kikosi msimu huu.

kutoka juu koshoto ni Tom Starke (mlinda mlango), Lulas Raeder (mlinda mlango), Claudio Pizarro, Dante, Emre can, Xherdan Shaqiri na Mitchell Waiser

TUPO PAMOJA FESTIVAL IN NÜRNBERG



Ni tamasha la kujitolea (none-profit) ambalo limeandaliwa na kijana mtanzania anayeishi katika mji wa Nürnberg nchini ujerumani, na linatarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya tarehe 29 mwezi huu. Lengo la tamasha hili ni kukusanya michango kwa ajili ya kuendeleza kituo cha watoto waliotokea katika mazingira magumu na wenye vipaji. Kikubwa zaidi kinachofanyika ni kukuza na kuendeleza vipaji vyao ili waweze kujiajiri wenyewe katika maisha yao ya baadae.


Vilevile tamasha hili litakuwa ni sehemu ya kukusanya michango kwa ajili ya kuwafanya walimu na walezi wa watoto hao waweze kujikimu kimaisha. Ikumbukwe pia vifaa vya michezo kama mipira, viatu na jezi ambazo zipo katika hali nzuri zinapokelewa kwa ajili ya kuzituma Tanzania kusaidia watoto hao. Bila ya kusahau vifaa vya muziki kwa mfano magitaa, vinanda na kadhalika pia vinapokelewa wakati wowote hata baada ya tamasha.



Mratibu wa shughuli nzima bwana Eric ambae anafanya kazi hii kwa kujitolea akiwa katika moja ya hafla alizowahi kuziandaa katika kukusanya michango ya kusaidia kuinua vipaji vya watoto.


(Ratiba ya shughuli nzima)

Tamasha hili linatarajiwa kuanza majira ya saa saba mchana siku ya jumapili ya tare 29-07-2012 ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa ujerumani na wengine kutoka nje ya ujerumani.

Shughuli nzima itakamilishwa na burudani ya muziki kutoka kwa Dj Mukada kutoka Tanzania.Pia kutakuwa na maonyesho ya mavazi na mafunzo maalum ya kupiga ngoma kwa watoto na wakubwa.


(Dj Max akicharaza Ngoma)

Badala ya kupiga muziki wa mashine kama ilivyozoeleka siku hiyo Dj Max atarudi katika asili yake na kucharaza ngoma za asili na kuuthibitishia umma kuwa yeye ni Mzaramu halisi wa Bagamoyo. usikubali kuhadithiwa, njoo ujionee mwenyewe.


KIINGILIO NI BURE,  NYOTE KARIBUNI!!!

Sunday, July 22, 2012

STAR OF THE WEEK, ABUBAR KAABUNGA FROM UGANDA WHO LIVES IN AUGSBURG (BAYERN) GERMANY



(utamu wa kushinda)

Kaabunga was born in Kampla Uganda and move to Augsburg (Bayern) Germany many years ago. He is a super fighter (KICKBOXER). He worn German Championship, European Championship and he is a World Champion in W.I.K.A



ABUBAKAR KAABUNGA AKIWA NA MASHABIKI WAKE BAADA YA USHINDI



(Abubakar with his team)

Many people in Germany,  Europe and the world know Mr. Kaabunga and respect him very much for what he is doing in Kickbox, he is a very talented boy. But its very sad that his own country Uganda just ignore him, especially the Kickboxing Federation of Uganda. They pretend like they dont know him, they dont know what he is doing, and even dont want to know his contribution in Kickbox. Thats very sad




Even though the Uganda Kickboxing Federation ignores him but whereever he goes for fighting, he always brings his national flag with him. Kaabunga says that he loves his country "Uganda" very much



TO BE A WORLD CHAMPION IS NOT A SMALL THING, LETS SUPPORT OUR BOY, LETS SUPPORT KAABUNGA. 




Friday, July 20, 2012

SAV CLAN WAACHIA KIOO KIPYA

AMIRI KOBA MATIGA, MWANABAGAMOYO ALIYEPANIA KUIVUMISHA SAUTI YA NGOMA DUNIA NZIMA





Tunapoizungumzia sanaa ya ngoma za asili na Sarakasi basi hatutomaliza kauli zetu bila ya kuhusisha jina Matiga. Ambaye ni kijana mdogo mwenye asili ya Bagamoyo na mzaliwa wa wilaya ya Bagamoyo mkoani pwani. Amekuwa akitangaza utamaduni wa Tanzania kwa juhudi zake binafsi nje ya mipaka ya tanzania. 

Pia aliwahi kushiriki katika "program" maalum ya mabadilishano ya vijana ya kitamaduni kati ya Tanzania na Norway. Mradi huo ujulikanao kama SPOR nchini tanzania unasimamiwa na Flame Tree Media Trust chini ya uongozi wa bwana Mwanzo Laurent Milinga 





Matiga (aliyekaa chini mbele) akiwa na washirika wake baada ya onyesho nchini Marekani wakiwa katika pozi la picha ya Pamoja.

Pamoja na kuishi kwa Obama lakini matiga bado anaendeleza sanaa yake kwa hali na mali na hivi karibuni anatarajia kufanya ziara kubwa sana barani ulaya




Mtoto wa Bagamoyo akiwa jukwaani anaonyesha manjonjo yake katika moja ya maonyesho yake




Pamoja na kuishi majuu lakini Matiga bado anaishi maisha yake halisi aliyokulia ya kitamaduni, hapa alikuwa anapika chapata badala ya kujichanganya kwenye migawaha ya kifahari.





Thursday, July 19, 2012

FRANK RIBERI AJIUNGA AANZA MAZOEZI NA WENZAKE RASMI



Ribery akilingisha uzi mpya wa Fc Bayern


Mchezaji machachari, ambae ni mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Fc Bayern yenye makazi yake mjini munich nchini ujerumani. Mchezaji huyo raiwa ufaransa leo amejiunga rasmi na wenzake walio kambini kwa maandali ya msimu ya msimu ujao wa ligi kuu ya ujerumani"BUNDESLIGA" . Pia ikumbukwe kuwa bayern Munich wanakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya mahasimu wao wakubwa " Dortmund" pia ya ujerumani katika wiki chache zijazo.

Katika kipindi cha misimu miwili ya ligi ya ujerumani  "BUNDESLIGA" timu ya Dortumund imekuwa ikibahatisha kuwafunga Fc Bayern licha ya mchezo mzuri unaonyeshwa na wekundu hao wa ujerumani.

Mchezo kati ya Fc Bayern dhidi ya Dortumund utafanyika ndani ya uwanja wa Allianz Arena, ikiwa ni fainali ya super cup, mnamo tarehe 12 August 2012

SUPER COMEDIAN FROM TANZANIA, MPOKI A.K.A MWARABU WA DUBAY AACHIA SONGI JIPYA

Wednesday, July 18, 2012

FC BAYERN YAFANYA MAUAJI YA KIKATILI


YAWACHARAZA TRENTIONO MAGOLI 11 BILA HURUMA



Mshambulia mwenye mbwembwe za kipekee Arjen Robben  akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Trentino ya Itally walipokuwa wakicheza mechi ya kirafiki nchini Itally hapo jana ambapo Fc Bayern waliibuka na ushindi wa Magoli 11 kwa duara



Beki wa kushoto wa fc Bayern ambaye ni kijana mdogo na mwenye kasi ya ajabu David Alaba akiwapeleka  puta mateja wa kitaliano



Monday, July 9, 2012

ALLY KIBA AITEKA MUNICH



Mashabiki wakiwa wamewehuka kwa furaha wakifurahia burudani ya Kiba





Wadau kutoka Holland, Sunday na James wakiwa wamezungukwa na warembo wa Stuttgart amabao pia walikuwepo kushuhudia show ya Single boy jijini Munich





Kiba akiwaimbisha mashabiki kwa mzuka





Single boyz from Munich





Msimamizi wa shughuli nzima Dj Max akiwa na dada Masi





Wakongwe wa jiji la Munich, Dj Kareem (left) na Dj Juma wakiwa wanakula raha 





WAREMBO!!!!!!