Sunday, September 30, 2012

BAADA YA KIMYA KIREFU "CHIDI BENZ" AFUNGUKA

MUANZILISHI WA BONGO FLEVA APATA MTOTO



Miongoni mwa wasanii wa awali kabisa kutambulika katika ramani ya muziki wa kizazi kipya mwanzoni mwa miaka ya tisini, Joseph Mbilinyi "Mr too proud au Sugu" ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kupitia chama cha Chadema. Sasa amekuwa baba baada ya mwenyezimungu kumjaalia neema ya mtoto.

Pia ifahamike kuwa Sugu ndio msanii mwenye Album nyingi zaidi kuliko kuliko msanii mwingine yoyote wa bongo fleva. Vilevile ni msanii wa kwanza kutoa album na ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza wa bongo fleva kupata nafasi ya kupiga "show" barani ulaya



Huyu ndiye mtoto wa Sugu, kwa jina anaitwa Sasha. Mungu ambariki na kumkuza vizuri


Thursday, September 27, 2012

RICK ROSS KUFANYA BONGE LA SHOW DAR ES SALAAM




Habari zilizothibitika muda mchache uliopita zinasema kuwa msanii kutoka nchini Marekani "Rick Ross" ndiye msanii wa kigeni atakayetumbuiza kwenye kilele cha Tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Media, linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 6 Oktober 2012.

Wednesday, September 26, 2012

FILAMU MPYA YA MAREHEMU KANUMBA SASA IPO MADUKANI




Ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu kifo chake, aliyekuwa muigizaji wa mahiri "Bongo Movies" Steven Charles Kanumba (The Great). Tayari kuna filamu ambayo aliicheza siku chache kabla ya kifo chake ambayo inakwenda kwa jina la "NDOA YANGU" sasa imeingia madukani ikiwa inasambazwa na steps. Kulingana na uhalisia hii ndio filamu ya mwisho kuchezwa na Kanumba kwa kuwa sasa hatunaye tena duniani.


MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU

Tuesday, September 25, 2012

OLIC NA MANDZUKIC WALIJITABIRIA KUWA WATABADILISHANA TIMU???



Mara ya mwisho walipokutaka katika uwanja wa Allianz Arena msimu uliopita wa ligi ya Ujerumani (Bundesliga). Wachezaji Mario Mandzukic na Ivica Olic walikuwa wakichezea timu mbili tofauti na wanazocheza sasa. Ambapo Olic alikuwa Fc Bayern Munich na sasa amehamia Wolfsburg, na Mandzukic alikuwa VfL Wolfsburg na sasa amehamia Bayern. Jioni ya leo wawili hao wanatarajia kukutana tena kwenye uwanja wa Allianz Arena kwa mara nyingine wakiwa wamebadilishana timu. 

Wachunguzi wa mambo wanajiuliza je, walipobadilishana jezi katika msimu uliopita ni kama walikuwa wakitabiri kuwa watabadilishana timu baada ya msimu wa ligi kuisha? au kila mmoja alikuwa anaitamani timu ya mwenzie? kwa maana Olic alikuwa anatamani kuchezea Wolfsburg na Mndzukic alitamani kucheza Bayern???


Saturday, September 22, 2012

DIAMOND AIBIWA VIATU, KOFIA MPAKA SOKS DODOMA... LAKINI BADO AENDELEA NA SHOW BILA KUJALI

JAY MOE ATUA STOCKHOLM!!!! TAYARI KWA MAKAMUZI



Msanii wa Bongo Jay Moe a.k.a Mr, Mchopanga wakwanza kulia akiwa na masharobaro wa jiji la Stockholm pia wachezaji wa zamani wa the big team "Simba Sports" ya Dar. Kutoka kushoto ni Shekhan Rashid na Athuman Eid Machupa.

Habari za uhakika zinasema kuwa Jay Moe anatarajia kufanya makamuzi ya ajabu ndani ya jiji la Stockholm siku ya ijumaa ya tarehe 28 September 2012 kuanzia mida ya saa nne usiku mpaka majogoo.



KARIBU WEWE NA MWENZIO


DAVID ALABA APATA NAFUU




Lile jembe la ukweli kutoka kijiji cha vipaji maeneo ya Säbenerstr jijini Munich, makao makuu ya chama kubwa Fc Bayern. Kijana mwenye umri mdogo kuliko wote katika kikosi cha kwanza David Alaba ameanza kupata nafuu kutokana na majiraha aliyoyapata kwa zaidi ya mwezi sasa.

Alaba aliwadhihirishia mashabiki kuwa anaendelea vizuri pale alipoingia mazoezini asubuhi ya leo na kupasha misuli kwa kukimbia hapa na pale huku akiwasalimia mashabiki waliohudhuria mazoezini hapo.

Friday, September 21, 2012

NANI KUIBUKA MISS TEMEKE LEO???




Kusini mwa jiji la Dar es Salaam pembezoni mwa bahari ya hindi maeneo ya mtoni sabasaba kwenye ukumbi wa PTA. Jioni ya leo patamalizika ubishi wa kuwa ni nani atavalishwa taji na kuwa Miss Temeke 2012/13

Kama picha inavyojionyesha hapo juu, hao ni washiriki wa Miss Temeke ambao ni warembo waliorembeka hasa

ONLY 24 HRS REMAING TO GO.... OKTOBERFEST IN MUNICH




This is how the main gate  looks like by night



CHEERSS!!!!!!!!!!!!!!!




Wednesday, September 19, 2012

Tuesday, September 18, 2012

NGOMA AFRIKA BAND WAACHA GUMZO BREMEN


Ras Makunja na vijana wake wakiwasha moto

Ni kundi la muziki wa dansi linaloundwa na vijana wa ki Tanzania kwa kushirikiana na vijana wenzao kutoka Congo ambapo wote kwa pamoja wanaishi nchini ujerumani. Chini ya uongozi wa Captain Ras Makunja (mtanzania) juzi waliacha wakizungumziwa baada ya kutoa show ya nguvu katika mji wa Bremen nchini ujerumani. Kwa hakika walikonga nyoyo za mashabiki wariohudhuria na pia kuwakumbusha nyumbani wazungumzaji wa lugha ya kiswahili pale walipoimba nyimbo za kiswahili. Yani ilikuwa ni burudani ya aina yake.



Baadhi ya masahbiki waliohudhuria wakiserebuka na kujimwaga uwanjani kuburudika na burudani tamu ya Ngoma Afrika Band


Monday, September 17, 2012

PREZZO ABONGA NA SALAMA WA MKASI BAADA YA BIG BROTHER

J.B AMPIGIA SALUTI MPOKI WA ORIJINO KOMEDI




Ilikuwa ni kwenye Tamasha la Fiesta mjini morogoro, ndipo muigizaji maarufu Jcob Steven (mwenye fulana nyeupe wa kati) aliposhindwa kujizuia na kujikuta akienda kumwagia minoti baada ya kumvunja mbavu kwa vichekesho vyake. Mchekeshaji anaejulikana kwa jina la Mpoki kutoka kundi la Orijino Komedi au ukipenda unaweza kumwita mwarabu wa Dubay, maarufu kama mwarabu wa Libya au mwarabu mweusi, kwa kuokoa muda mwite bepari wa kihaya.

Sunday, September 16, 2012

DJ DULLY BOY KUWASHA MOTO NDANI YA MEMMINGEN NEXT SATURDAY



Jumamosi ijayo ya tarehe 22 Sptember 2012, mji wa Memminge katika jimbo la Bayern utakuwa na burudani ya muziki usiopimika kutoka kwa Dj Dully boy na Dj Rama. Bila kusahau the Most wanted "Dj Max" pia atawakilisha.

Burudani hii ni kuanzia mida ya saa tatu usiku mpaka asubuhi, pia kutakuwa na chakula cha ki Africa na vinywaji mbalimbali. Zawadi maalum zitatolewa na Mambo Bado sounds na Dj Max Entertainments kwa mwanadada atakaependeza kuliko wote, pia kwa watu watatu watakao cheza vizuri zaidi.

KARIBUNI SANA!!!!

ONLY 6 DAYS REMAINING... JAVI MARTINEZ IS READY FOR OKTOBERFEST




Ikiwa zimebaki siku 6 tu kuelekea kwenye Festival kubwa kuliko zote katika jimbo la Bayern (Oktoberfest), tayari kiungo mpya wa Fc Bayern "Javi Martinez" ameshanunua mavazi ya asili ya kibavaria kwa ajili ya tamasha hilo.

Tamasha hili hufanyika kipindi kama hiki kila mwaka kwa takriban muda wa wiki mbili na nusu, na kwa mwaka huu litaanza rasmi siku ya jumamosi ijayo 22 Sep 2012 mpaka tare 7 Okt 2012. Tamasha hili la wanywa Pombe linalojulikana kama Oktoberfest litafanyika maneneo ya Theresienwiese katika jiji la Munich.

MASHABIKI JINSI WALIVYOMCHOKOZA DIAMOND KWA KUTAJA JINA LA WEMA ALIPOIMBA KWENYE FIESTA DODOMA

Saturday, September 15, 2012

HAPPY BIRTHDAY TO YOU " DJ LADY KIARIE"




The Dj Max Entertainments and the crew wish you a happy birthday, we are very happy to work with you. May God bless you on this special day and forever. with lots of Love from my self (Dj Max). Me and my crew together we say 
HAPPY BIRTHDAY

Monday, September 10, 2012

BAADA YA BILBAO KUTAKA KUMUWEKEA NGUMU MARTINEZ HATIMAYE AANZA MAZOEZI RASMI NA FC BAYERN



Kifaa kipya cha Fc Bayern kikiwa kinatokea Bilbao, ambapo usajili wake almanusura ulete utata na labda asingeweza kuchezea nyota nyekundu ya kusini (FC BAYERN) hatimaye kila kitu kipo sawa na leo ameanza mazoezi rasmi. 

Picha juu inaonyesha akiwa na Bastian Schweinsteiger (kushoto) baada ya mazoezi wakibadilishana mawazo

Sunday, September 9, 2012

JUMA NATURE BADO NI NOMA!!!! AFUNIKA FIESTA TABORA KINOMA NOMA



Anaitwa Juma Kassim Kiroboto, mtoto wa Temeke jijini Dar. Ingawa wengi hupenda kumuita Juma nature au Sir nature. Pamoja na kuwa hajadondosha songi jipya kwa muda mrefu kidogo lakini pindi anapopanda jukwaani huwatia uchizi mashabiki wake wa masongi yake ya kitambo. Bado kuna watu wanajiuliza je? anatumia kizizi?

"Huyu jamaa hajatoa wimbo mpya lakini alipopanda tu watu wote walichanganyikiwa kwa furaha, sijui ana kizizi" moja ya mashabiki alisikika akisema baada ya tamasha la Fiesta lililofanyika mjini Tabora ambalo liliandaliwa na wakali wa burudani nchini Tanzania Clouds radio (the people station)

Saturday, September 8, 2012

JULIA NJOROGE FROM KENYA IS MISS EAST AFRIKA BELGIU 2012



Kwa niaba ya The Dj Max Entertainments and the crew, tunakupa hongera sana dada yetu kwa kushinda taji la Miss East Africa Belgium. Hongera pia kwa waandaji bila za kumsahau Azam, Kitokololo na the big bosss Denis Ruba

Wednesday, September 5, 2012

EAST vs WEST AFRICA PARTY IN MUNICH ILIKUWA NOMAA!!!!!


Super Dj Rama akifanya makamuzi



Bobby St akiwarusha mashabiki


Wadada warembooo!!!!!!!!!



Dj Lady Kiarie..... One Love!!!!



Cute girls


Just chilling and Enjoying



Mashabiki wakiburudika na kuburudishwa na Bobby st



Doctor Kingo in the house!!!!!!!  kaka rudi kazini wagonjwa watakufa



Hapa nimejichanganya na wenye Munich yao




NYOMI ZAIDI YA LILE!!!!!



HAPPY BIRTHDAY MATHIAS SAMMER (ZUM GERBUSTAG VIEL GLÜCK)




Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya ujerumani na ambae pia aliwahi kuichezea Dortmund, lakini kwa sasa ni kiongozi katika bodi ya michezo kwenye chama kubwa FC BAYERN MÜNCHEN. Herr Mathias Sammer leo amezaliwa na kwa pamoja tunasema "Zum Geburtag viel Glück "

Tuesday, September 4, 2012

MWANAKIJIJI ACHANGANYIKIWA KWA FURAHA YA KUKUTANA NA SHAFFIH DAUDA, MBWIGA WA MBWIGUKE (MZARAMU HALISI) NA BONGE

BI KIDUDE HAJAFAAAA!!!!! WACHENI KUMZUSHIA




Msanii maarufu na mzee kuliko wote Afrika mashariki, ambae ni mzaliwa wa Zanzibar katika Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA). Fatma bint Baraka maarufu kama bi Kidude alizushiwa kuwa amefariki mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa za sahihi kutoka kwa wajukuu zake zinasema kuwa bibi bado yuhai  na kwa uwezo wa mungu ataishi maisha marefu zaidi japokuwa kwa sasa afya yake si nzuri kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hawakuyataja. "Maradhi ni kitu cha kawaida na kila binaadamu huugua, ni kweli bibi anaumwa lakini hajafa na tunamuombea kwa mungu apate afueni" hayo yalisemwa na mjukuu wake ambaye pia ni msanii wa miondoko ya mduara kutoka visiwani nilipoongea nae kwa njia ya simu, lakini aliomba jina lake lisiandikwe hapa, nami nafanya hivyo kwa kumuheshimu na kuheshimu mawazo yake.