Thursday, January 31, 2013

FILAMU YA MWISHO ALIYOCHEZA SHARO MILLIONEA KUWA MITAANI KESHO



Hussein "Sharo Milionea" enzi za uhai wake

Taarifa za kuaminika kutoka kwa familia ya "King Majuto" pamoja na Sharo zimetufikia hivi punde kuthibitisha kuwa ile filamu ya vichekesho aliyocheza Sharo siku chache kabla ya kukumbwa na umauti ambayo inajulikana kwa jina la "KITU BOMBA" itakuwa kitaani kesho. Akithibitisha hilo kwa njia ya simu mtoto wa King Majuto na ambae ndio meneja wake, Hamza Majuto amesema kuwa filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na kampuni ya Steps duniani kote.


Hili ndilo kava la filamu hiyo mbele na nyuma

Pia jioni hii Hamza Majuto aliandika katika ukurasa wake wa face book kuwa watu wakae mkao wa kula kwani kazi imeshapikwa, ikapikika na kuiva hivyo basi wananchi pamoja na mashabiki wa filamu za vichekesho wasubiri burudani tu.


King Majuto

Hata hivyo juhudi za Makusudi za kumpata King Majuto ili azungumze japo machache kuhusu ujuio wa filamu hiyo ziligonga mwamba kutokana na kuwa ametingwa na shughuli nyingi za kujenga taifa.



Wednesday, January 30, 2013

KITALE ATANGAZA NDOA



Hamisi Kitale kwenye pozi la kazi

Msanii maarufu wa filamu za vichekesho Afrika Mashariki "kitale" ambaye amepata umaarufu sana kwa "style" yake ya uteja hivi karibuni amevunja ukimya na kufunguka kuwa  anatarajia kufunga ndoa siku ya jumapili ijayo. Akiongea na washkaji zake wa karibu kitale alisema katika maisha yake amepitia matatizo mengi na amekutana na changamoto za aina mbalimbali. Hivyo ameamua kuoa na kutulia kujenga familia iliyo bora. The Dj Max Entertainments tunampongeza na kumuombea kila la heri katika ndoa yake

Wednesday, January 23, 2013

SERENA WILLIAMS ATOLEWA JASHO NA CHIPUKIZI WA MIAKA 19

HUSSEIN MACHOZI: "NILITAMANI KUWA MCHEZAJI MAARUFU LAKINI MAISHA YAMENIFANYA NIWE MWANAMUZIKI MAARUFU"



Mwanamuziki maarufu wa "Bongo fleva" leo hii amefunguka alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Leo tena cha Clouds fm. Akielezea historia ya maisha yake na shida alizokutana nazo mpaka kufikia hapo alipo leo hii, hadi kufanya jina lake halisi la Hussein Rashid kubadilika na kuwa "HUSSEIN MACHOZI"

Akielezea ndoto zake za kucheza timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania pia alifunguka kwa kusema kuwa kocha msaidizi wa sasa wa timu ya taifa (Jina kapuni) ndiye aliyevunja ndoto zake za kuendeleza kipaji chake cha mpira wa miguu wakati akiwa timu ya Kagera Sugar. Miongoni mwa vitu alivyokuwa akifanyiwa na kocha huyo na kumkatisha tamaa ni kupewa nguo za kocha huyo ali amfulie wakati wachezaji wengine wakiendelea na mazoezi.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa bado anaupenda sana mchezo wa mpira wa miguu kuliko muziki lakini hali ya maisha kwa sasa hamruhusu, labda kama atapata timu ambayo itamlipa vizuri.

NEW MUSIC VIDEO: KEISHA ft DIAMOND "NIMECHOKA"

Thursday, January 17, 2013

kama ulikosa kusikiliza dondoo za bundesliga tarehe 17 january, hii hapa

PROFESA JAY AWACHIMBIA MKWARA WASANII CHIPUKIZI



"Machipukizi msitukane Wakunga kwa kuwa mnasifiwa kuwa wakali kwa hiyo album moja, Tutaongea lugha moja mkiwa na album ya tano...MMENIELEWA??"

Maneno hayo juu ndio ilikuwa status ya kwenye ukurusa wa facebook ya mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Josseph Haule maarufu kama Prosefa Jay. Ingawa hakufafanua kwa undani zaidi alimaanisha nini lakini watafiti wa mambo wanadai ni kuwa alikuwa anawatahadharisha madogo wasijisahau kutokana na umaarufu ambao wameanza kuupata juzijuzi.

Wednesday, January 16, 2013

BREAKING NEWS!!!! PEP GUARDIOLA KOCHA MPYA BAYERN KUANZIA MSIMU UJAO



Raia wa Spain mwenye umri wa miaka 41 leo ametangazwa rasmi na uongozi wa Fc Bayern Munich ya Ujerumani kuwa ndie atakaekuwa mrithi wa Jupp Heynckes kwa nafasi ya ukocha. Heykes ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu wa ligi alikataa kuongeza mkata kwa madai kuwa anahitaji kupumzika kutokana na umri na hivyo uongozi wa Bayern ukaona kuwa anaefaa kwa nafasi hiyo si mwingine bali ni Pep Guardiola.

Tuesday, January 15, 2013

MSANII LADY JAY DEE AMALIZA SALAMA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania na pia mmiliki wa kundi la muziki la Machozi Band, Judith Wambura "LADY JAY DEE" ukipenda unaweza ukamwita Jide. Amemaliza salama safari yake ya siku sita ya kukwea kilele cha mlima mrefu kuliko yote barani Afrika "Mlima Kilimanjaro" akiwa ameongozana na mumewe pamoja na mpiga picha wao. Mara baada ya kushuka kutoka kileleni walikabidhiwa vyeti maalum vya uthibisho kuwa wamefika kilelena. Vyeti hivyo walikabidhiwa na muhifadhi mkuu wa mlima huo.

Thursday, January 10, 2013

THE NEW HASHEEM THABEET

SIMBA WAWASILI NCHINI OMAN KWA MAANDALIZI YA LIGI




Baadhi ya wachezaji wa simba walipowasili nchini Oman, wakiwa wanajisajili katika Hoteli waliyofikia yenye hadhi ya 5 star iitwayo Almadinah Holiday. Timu ya Simba itapiga kambi nchini Oman kwa muda wa wiki mbili kufanikisha maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya mpira wa miguu Tanzania Bara (Tanganyika)

Wednesday, January 2, 2013

HUYU NDIO JAMAA ALIYEFANYA DIAMOND ARUSHIWE CHUPA, VITI NA MAYAI YALIYOOZA AKIWA JUKWAANI (ANAITWA PAPAA)

R.I.P SADIKI JUMA KILOWOKO (SAJUKI)


Aliyekuwa mwgizaji maarufu wa Bongo Movie nchini Tanzania na ambaye pia ni Mume wa Star mwingine Wastara Juma hatunae tena Duniani. Habari za kuaminika zinasema kuwa Sajuki amefariki dunia Alfajiri ya leo. Bwana ametoa na bwana ametwa, Jina la bwana litukuzwe.