Sunday, May 26, 2013

MARIO MANDZUKIC, AWEKA HISTORIA KUWA RAIA WA KWANZA WA KROATIA KUFUNGA GOLI KWENYE FAINALI ZA CHAMPIONS LEAGUE



Ni mzaliwa wa Slavonski Brod nchini Kroatia ambaye ana umri wa miaka 27, kwa maana ya kuwa alizaliwa mwaka 1986 mwezi mei tarehe 21. Nyota yake imeanza kumeremeta zaidi msimu huu wa Bundesliga alipojiunga na FC Bayern akiwa anatokea Wolfsburg.Alizidi kujiongezea umaarufu siku hadi siku kwa umahiri wake wa kufunga angalau goli moja katika kila mechi aliyocheza na jana ameandika historia kuwa raia wakwanza kutoka Kroatia kupachika goli kwenye fainali za mabingwa wa Ulaya.

Friday, May 10, 2013

FC BAYERN WATAMBULISHA JEZI ZAO MPYA

KUTOKA NCHINI UTURUKI, MWAMUZI CUNEYT CAKIR NDIO ALIYECHAGULIWA KUCHEZESHA MECHI YA FAINALI YA MABINGWA WA ULAYA!




Ni raia wa uturuki ambae anasifika kumudu mikikimikiki ya mapambo kadhaa ya mpira wa miguu, pia huwa hana mzaha kwani ni mkali wa kutoa adhabu kali kama ambavyo picha inaonesha. Anaitwa Cuneyt Cakir ndio atakae kuwa mwamuzi siku ya tarehe 25 mwezi huu kunako dimba la Wimbley nchini Uingereza ambapo Nyota Nyekundu ya Kusini "The Bavarians" F.C BAYERN MÜNCHEN watakuwa wakitoana jasho na nyuki wa kaskazini magharibi BORUSSIA DORTMUND kuwania ubingwa wa kombe la ulaya.

NI DAKIKA TATU NA NUSU TU ZA VIDEO MPYA JAGUAR "KIPEPEO" KUTOKA NAIROBI KENYA

Wednesday, May 1, 2013

HUYU JAMAA NI BINAMU YAKE RIBERY AMBAE KWA MIAKA MINGI HAWAELEWANI KUTOKANA NA TABIA ZAKE ZA KIHUNI




Mpaka hivi sasa jina lake kamili halijafahamika, lakini ana mahusiano ya kibinamu na Ribery. Mara kadhaa amekuwa akimsumbua kwa kumfuata mazoezini, kambini au kwenye mechi ili kumuomba msamaha lakini hakuwahi kupata nafasi hiyo. ni mtoto ambaye familia inamuona kama mtukutu na kumchukia lakini baaada ya ushimdi na kuingia fainali kwa mara ya kwanza Frank Ribery alimuonesha tabasamu binamu yake na kumpa jezi.